Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataka vipimo vya tezi dume Kambi ya Afya

50868 Pic+tezi+dume

Sun, 7 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Waandaaji wa huduma ya vipimo vya afya bila malipo kupitia "Mwananchi Kambi ya Afya" wameshauriwa kuanzisha vipimo vya tezi dume kwa huduma ijayo.

Wamesema elimu ya  ugonjwa huo ilitangazwa kwa kasi, hivyo wengi wangetamani kupata huduma ya vipimo vyake hususani iwafikie watu wa hali ya chini.

Khalid Ahmed (54), mkazi wa Kinondoni Moscow ameshauri katika awamu nyingine ya huduma hiyo, waandaliwe pia wataalamu wa vipimo vya tezi dume ili kujua mapema hali zao.

Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 6, 2019 wakati wa utoaji huduma kupitia kambi hiyo inayofanyika katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.

"Vipimo vya tezi dume tunasikia ni gharama sana, mie nilikuwa nimejiandaa kupima na tezi dume, kwa hiyo ningeshauri kambi ijayo watuletee hiyo ya tezi dume, lakini si mbaya nimenufaika na vipimo vinne bure ambavyo pengine ningelipia sehemu nyingine,’’ amesema Ahmed.

Yakobo Joseph (32), mkazi wa Kinondoni Mkwajuni amepongeza huduma zinazotolewa katika kambi hiyo, akisema ni jambo la kuigwa na taasisi nyingine.

"Nimefika hapa saa 7:00 mchana, nimepima vipimo vinne, kwa sasa ninapima kwanza macho banda la CCBRT, nimegundua kuna nyama ndani ya macho, "amesema Joseph.

Kambi hiyo yenye kauli mbiu "Afya kwa Wote", imeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited chini ya udhamini wa taasisi mbalimbali zikiwamo Aghakan, TFNC, Pharmacy Council pamoja na benki za CRDB na KCB.

Taasisi 19 zinazohusika na huduma za afya zimeshiriki kutoa huduma kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza.



Chanzo: mwananchi.co.tz