Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watafiti wakataa nyama kuhusishwa zaidi na saratani, kisukari, ugonjwa wa moyo

78001 Moyo+pic

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Washington, Marekani. Kupunguza ulaji nyama nyekundu ni ushauri wa kawaida wa madaktari kwa ajili ya kuzuia saratani na ugonjwa wa moyo -- lakini mapitio ya tafiti nyingi yanaonyesha kuwa hatari hiyo ni ndogo na ushahidi hauko bayana.

Katika mwongozo mpya uliochapishwa jana Jumatatu katika jarida la afya la Annals of Internal Medicine, jopo la watafiti kutoka nchi saba limeshauri kwamba "watu wazima waendelee na ulaji wa nyama isiyochakatwa".

Ushauri huo -- ambao muda mfupi baada ya kutoka uliamsha mjadala kutoka kwa wataalamu -- uliongeza kuwa watu wazima wanatakiwa "waendelee na tabia ya sasa ya kula nyama iliyochakatwa".

Utafiti huo uliochapishwa hilo linalohaririwa na Chuo cha Wataalamu wa Viungo wa Marekani (American College of Physicians), umechambua tafiti kadhaa, kuziweka pamoja kupunguza kula nyama mara tatu kwa wiki kunaweza kushusha vifo vya saratani hadi watu saba kati ya 1,000.

Watafiti hao wanasema kushuka kokote kwa aina hiyo ni kwa kawaida na kwamba wamebaini kuwa kuwepo kwa uwezekano mdogo wa uhakika kuhusu takwimu hizo.

Waliongeza kuwa ubora wa ushahidi unaohusisha nyama na magonjwa ya moyo na kisukari ni "mdogo sana".

"Kuna hatari ndogo ya saratani, ugonjwa wa moyo na kisukari, hata hivyo, ushahidi hauna uhakika," alisema Bradley Johnston, profesa katika Chuo Kikuu cha Dalhousie cha Canada na mkurugenzi wa taasisi ya NutriRECS ambayo iliandaa mwongozo huo, alipoongea na AFP.

"Kwa hiyo, kunaweza kukawa na kupungua au kunaweza kusiwepo.

"Watu wanatakiwa wafanye maamuzi yao. Tunawapa makisio bora ya ukweli."

Nyama za kuchoma, soseji?

watafiti hao walisema wanataka kubadili mtazamo wa kizamani wa kutoa ushauri kiujumla, na kujikita zaidi katika ushahidi wa faida mojamoja.

"Watu wanbatakiwa kuangalia haya na natumaini wafanye maamuzi yao wakiwa wana ufahamu zaidi kuliko kuambiwa nini cha kufanya na taasisi za kitaalamu," alisema Johnston.

Lakini kula nyama kidogo na iliyochakatwa kumekuwa ni nguzo ya mwongozo wa ulaji kiafya kwa miongo mingi katika nchi nyingi na taasisi zinazotoa ushauri wa kiafya.

Chanzo: mwananchi.co.tz