Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataalamu waeleza tofauti ya kuwekwa karantini na mtu kutengwa

99691 Pic+karantini Wataalamu waeleza tofauti ya kuwekwa karantini na mtu kutengwa

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Tangu kuingia kwa ugonjwa wa virusi vya corona (Covid-19,) kumekuwa na mkanganyiko kati ya mazingira ya mtu kuwekwa karantini na kutengwa (isolation) katika maeneo maalumu.

Kituo cha Usimamizi na Udhibiti wa Magonjwa (CDC) kinasema karantini ni ile hali ya kumtenga mtu au kikundi cha watu wanaoaminika wamekutana na magonjwa ya kuambukiza na wale walio salama.

Kwa mujibu wa CDC, hao wanaowekwa kwenye karantini wanakuwa katika hatari ya magonjwa ya kuambukiza kama Covid-19 au wameonyesha dalili au hawajaonyesha.

Hao huwekwa katika eneo maalumu la uangalizi ili kuwazuia kugusana kwa namna yoyote na wengine ambao hawajapia mazingira hayo ili kuzuia uwezekano wa kusambaa kwa maambukizi.

Kwa hiyo watu wanawekewa karantini wakati wakiwa hawaumwi kwa kuwa wanaweza kuwa na dalili fulani au kwa kuwa wanatokea nchi au maeneo ambayo tayari yana waathirika, inasema CDC.

“Sasa kutengwa au “isolation” tafsiri yake ni pale mtu au watu waliokuwa wamewekwa katika karantini wanapokuwa wamethibitishwa katika maabara kwamba wameambukizwa na hivyo kuwekwa peke yao ili wasiambukize wengine,” inaeleza CDC.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Dk Shita Samwel anasema mgonjwa anapokuwa amewekwa katika karantini, wataalamu wa afya huendelea kumwangalia na kuchukua vipimo mbalimbali.

“Huyu maana yake bado ni suspect (mshukiwa). Hapa wataalamu wanaendelea kumwangalia na kumpa ushauri,” anasema.

“Yaani anafanyiwa pia counseling (ushauri) asije akapata msongo wa mawazo au matatizo ya kisaikolojia na anapewa huduma zote wakati majibu yakisubiriwa.

“Lakini anapokuwa ametengwa maana yake tayari majibu yamerudi kuwa ameambukizwa na hapa ndio anaanza kupata matibabu na wanaomhudumia lazima wajikinge kikamilifu.”

Tangu kuibuka kwa virusi hivyo vinavyoitwa Covid-19, abiria wanaopita mipakani na kuonekana wana dalili za maambukizi, huwekwa katika karantini na wanaofanya haya ni lazima nao wajikinge kikamilifu.

Baadhi ya nchi, Kenya ikiwamo, zimeweka utaratibu wa kuwaweka katika karantini kwa siku 14 wageni wote wanaoingia nchini humo kutoka nchi zilizoathiriwa na Covid-19.

Kwa njia hiyo, watu wote ambao wamekutana na wagongwa waliothibitika kuwa na virusi vya corona wanawekwa karantini.

Chanzo: mwananchi.co.tz