Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataalamu wa afya wataka mabadiliko ulaji

432b701406c152522b808a1b3be0e3a2 Wataalamu wa afya wataka mabadiliko ulaji

Sun, 17 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MAGONJWA yasiyoambukiza yanasababisha vifo nchini kwa asilimia 33 ya vifo vyote hivyo wananchi wametakiwa kubadilisha mfumo wa maisha ikiwamo ulaji.

Sababu kuu za magonjwa hayo ni pamoja na mfumo wa maisha utokanao na lishe duni, kutokufanya mazoezi na hata matumizi ya vilevi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila,Dk Julieth Magandi wakati wauguzi wa hospitali hiyo walipoamua kutoa huduma bure ya kuchunguza afya pamoja na kupata ushauri kwa wagonjwa.

Huduma hiyo ya uchunguzi wa Afya ikiwemo magonjwa yasiyoambukiza imetolewa hospitalini hapo kwa siku tatu na zaidi ya wananchi 300 wamechunguzwa.

Akizungumza wakati uchunguzi ukiendelea, Dk Magandi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila), Profesa Lawrance Museru na kuwasisitiza wananchi kutambua kuwa wanalo jukumu la kulinda afya zao ili kuepuka magonjwa hayo.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2018 zinaonesha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanaelekea kuzidi vifo vitokanavyo na magonjwa yanayoambukiza duniani.

"Magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu,saratani, kisukari na hata magonjwa yanayoathiri mifumo ya upumuaji," alisema .

Aidha alisema kwa mujibu wa takwimu hizo, wagonjwa wa moyo na mishipa ya damu ni takribani milioni 17.9, saratani milioni tisa,magonjwa yanayoathiri mifumo ya upumuaji milioni 3.9 na kisukari milioni 1.6 kila mwaka.

Alisema athari za magonjwa yasiyoambukiza ni kubwa katika jamii na duniani kwa ujumla, takwimu za WHO kwa mwaka 2018 zinaonesha kila mwaka watu milioni 41 hufariki na katika hao asilimia 71 ya vivo vyote husababishwa na magonjwa yasihoambukiza.

Alisema takwimu zinaonesha asilimia 15 hufariki kati ya umri wa miaka 30 mpaka 69 ambapo asilimia 85 ni vifo kutoka nchi zenye uchumi mdogo na uchumi wa kati.Na kwa takwimu hizo Tanzania vifo vitokanavyo na magonjwa hayo ni asilimia 33 ya vifo vyote.

Kuhusu uchunguzi huo, alisema wauguzi wamejitolea kutimiza wajihubu wao katika Jamii kwa kupima Afya bure,kutoa elimu ya afya na maelekezo ya tiba stahiki kwa wanajamii watakabainika kuwa na viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza.

Alisema watakaogundulika kuwa na matatizo watapata fursa ya kumuona daktari bure bila malipo pamoja na huduma za ushauri wa kitabibu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi,Muhimbili Upanga, Zuhura Mawona aliwasihi wananchi kufuata maelekezo ya wataalam wa Afya,jambo litakaloweza kuwaepusha na magonjwa hayo

Chanzo: habarileo.co.tz