Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataalamu wa afya wasisitiza elimu zaidi ya usonji

Afcbe2dcee94ed0af06869bbbd5172bb Wataalamu wa afya wasisitiza elimu zaidi ya usonji

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wataalam wa kada ya afya nchini wameaswa kuongeza juhudi katika kuielimisha jamii juu ya ugonjwa wa usonji hatua itakayosaidia kuifanya jamii kuwa na uelewa wa kutosha na hivyo kuondoa tatizo la ubaguzi kwa watoto wenye ugonjwa huo.

Rai hiyo imetolewa juzi na Madaktari kutoka hospitali mbalimbali wakati wakishiriki mjadala kuhusiana na tatizo la usonji uliofanyika kwa njia mtandao na kuwahusisha madaktari mbalimbali chini ya uratibu wa Taasisi inayojihusisha na utoaji elimu kuhusu usonji ya 'Lukiza Autism Foundation'

Akizungumza kuhusu umuhimu wa elimu hiyo, Daktari kutoka hospitali ya TMH iliyopo Sinza, Isaac Maro alisema usonji ni tatizo kama ilivyo matatizo mengine linalohitaji uelewa wa kutosha kwa jamii ili kupunguza changamoto zinazokuwa watu wenye tatizo hilo.

Alisema kama watalaamu wote wa afya kwa umoja wao wataweka mkazo kwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa huo, ni wazi kutaifanya jamii hiyo kuwa na uelewa wa kutosha na hivyo kuwa karibu na watu wenye tatizo hilo.

"Tunapaswa kufanya kazi hii bila ya kuchoka, twende maeneo yote na kutoa elimu kwa wananchi..tukifanya hivyo tutawasaidia watu wengi kulielewa tatizo hili na hivyo kupunguza unyanyapaa dhidi ya wenye tatizo hilo mahali penye hali hiyo" alisema Dk Maro

Kwa upande wake Daktari wa magonjwa ya akili Paschal Kang'iria alisema elimu kuhusiana na usonji ndiyo suluhisho pekee litalowezesha kuleta mabadiriko katika jamii na kudai kuwa tofauti na hapo itakuwa sawa na kujidanganya

Aidha aliwashukuru waandaji wa mdahalo huo kwa kuwakutanisha madaktari mbalimbali na kujadiliana kuhusu ugonjwa huo na kusisitiza kuwa wao kama madaktari wana wajibu wa kuhakikisha wanaisaidia jamii kuwa na uelewa juu ya suala hilo.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Lukiza Autism Foundation Hilda Nkabe pamoja na mambo mengine alisema usonji ni tatizo linalohitaji hali ya ukaribu baina ya mwenye tatizo hilo na yule aliyenalo hasa wazazi.

Anasema kama wazazi wa watoto wenye tatizo la usonji watasimama imara na kuwa karibu na watoto hao, itawasaidia watoto hao kuongeza uelewa katika mambo mbalimbali na hivyo kupunguza tatizo inayojitokeza katika jamii.

Alisema katika kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha katika jamii, taasisi hiyo imeaandaa chakula maalumu cha jioni chenye lango la kukusanya fedha ambazo zitasaidia ununuzi wa vifaa mbalimba sambamba na kusaidia matibabu kwa watoto wenye tatizo.

Alisema hafla hiyo itakayofanyika leo katika hoteli ya Sapphire iliyopo Mbezi Beach na kuongozwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na watoto Doroth Gwajima itawahusisha watu kutoka makundi mbalimbali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz