Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataalamu tiba asili waonya matapeli covid-19

62f6139702ebf50f7fe081132151a301 Wataalamu tiba asili waonya matapeli covid-19

Thu, 11 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WATANZANIA wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya matapeli wa tiba za asili wanaojitokeza kuwa wao ni mabingwa wa kuweza kutibu ugonjwa wa Covid-19 kwa kipindi hiki ambapo serikali imehimiza watu wake kujifukiza kwa mimea ya asili.

Rai hiyo imetolewa na Said Mbogo na Benjamin Mzuri, ambao ni wataalamu wa tiba ya asili wakati wakizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na wimbi kubwa linaloweza kujitokeza la waganga wa tiba asili kuwa na uwezo wa kutibu ugonjwa Covid-19.

Walisema kuwa kutokana na waganga hao kuanza kuibuka kwa kipindi hiki ambacho serikali imetoa ruhusa ya kujifukiza, watanzania wanahitaji kuwa waangalifu na matapeli hao wanaofanya wana uwezo wa kutibu kwa kutumia mimea ya asili huku wakiwa na lengo la kujipatia fedha na mali kwa udanganyifu.

Mbogo amewataka waganga wa tiba asili kuhakikisha wanapata usajili ili waweze kutambuliwa kisheria na waaminiwe na serikali na wateja wanaowahudumia.

Kwa upande wake Mzuri ambaye ni mtalaamu wa tiba asili mkoani Dodoma ameiomba serikali kuanzisha kliniki ya tiba asili ili waweze kutambuliwa na kuwawezesha kuwasaidia watanzania walio wengi.

Alisema kliniki hiyo itaweza kuthibitisha dawa zinazotokana na mimea ya asili na mkemia mkuu na watumiaji kabla ya kuwahudumia wateja wao kwa ajili ya kuwalinda kiafya.

Aidha amekiomba chama cha waganga wa tiba asili kuwasimamia waganga hao ili waweze kupatiwa leseni ambayo itakayowawezesha kufanya kazi zao kwa uwazi na uhuru tofauti na ilivyo kwa sasa hivi ambapo wengi wao wanahusishwa na tabia ya utapeli.

"Rai yetu kwa upande wa serikali tunaiomba kujengewa kliniki ili dawa zetu zitambuliwe,pia itawezesha hata kuwatambua waganga ambao ni matapeli wanaoharibu kazi mzuri inayofanywa na waganga wa tiba asili,"alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz