Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataalamu: Maziwa ya mama ndiyo akili ya mtoto/iachwe

Nyonyo1 Ed.jpeg Haijakamilika

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: ippmedia.com

Ofisa Lishe Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Emmanuela  Lawrence, alibainisha hayo jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya   Wiki ya Unyonyeshaji uliofanyika kwenye Kituo cha Afya Ubwari, mgeni rasmi akiwa Diwani wa Genge, Moses Kisiki.

Alisema utafiti unaonyesha maziwa ya mama humfanya mtoto kuwa na akili na mwenendo mzuri katika kujifunza mazingira na uelewa mpya.

Lawrence alisema unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni muhimu kutokana na faida ambazo humpatia mtoto virutubisho vyote anavyohitaji kwa uwiano sahihi wa ukuaji na maendeleo yake.

Alisema maziwa ya mama pia humpatia mtoto kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama kuharisha na magonjwa ya mfumo wa hewa.

Ofisa Lishe huyo alisema maziwa ya mama ni safi na salama, hupatikana muda wote katika joto sahihi na yanakaa saa nane bila kuharibika katika joto la kawaida.

Lawrence alisema  pamoja na juhudi zinazofanywa kwa lengo la kujenga mazingira wezeshi kwa wanawake wanaonyonyesha, bado kuna vikwazo mbalimbali vinavyochangia kupunguza kasi ya unyonyeshaji katika jamii.

Alisema wazazi wengi  mara nyingi wanazingatia zaidi masuala ya kujifungua kuliko mambo muhimu baada ya kujifungua kama vile kunyonyesha, huku kukiwa na kikwazo cha uhaba wa wafanyakazi na watoa huduma za afya wanaopaswa kutoa elimu ili wanawake wajue umuhimu wa kunyonyesha.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Frola Kessy, alisema maziwa ya mama yana umuhimu mkubwa kwa mtoto,m akiwahimiza wazazi watimize wajibu wao kwa kuepuka kuwaachisha mapema ama kuwanunulia maziwa ya wanyama watoto wao.

Diwani wa Genge, Kisiki, alisema kinamama lazima wajenge utamaduni wa kunyoyesha watoto huku akiagiza watoa huduma za afya kutoa elimu kwa wazazi ili wajue wajibu wa kuwanyonyesha watoto wao.

Chanzo: ippmedia.com