Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataalam wa afya Kahama wapewa mafunzo ya corona

Afya.webp Wataalam wa afya Kahama wapewa mafunzo ya corona

Thu, 30 Apr 2020 Chanzo: --

SHIRIKA la World Vision Tanzania, kwa kushirikiana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, limetoa mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wataalam wa afya katika wilaya ya Kahama kwa lengo la kujilinda dhidi ya virus vya corona wakiwa kazini pamoja na kuwahudumia wagonjwa.

Akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo hayo ya siku tatu, meneja wa World Vision, Kanda ya ziwa, John Masenza, amesema katika kpindi hiki cha janga la corona shirika limeamua kuungana na serikali katika kapambana na virusi hivyo.

Amesema lengo ni kujengea uwezo wa wataalam wa afya kuwa na mbinu au uelewa wa kutosha juu ya namna ya kwahumudumia wagonjwa bila hofu yoyote pamoja na namna ya kujikinga wasiweze kuambukizwa virusi hivyo wakati wakiwahudumia washukiwa na wagonjwa.

"Sisi Kama wadau ya masuala ya jamii lazima tujikite katika kada hii ni muhimu sana na sisi kama shirika la world vision Tanzania tumeona ni vyema tukawakusanya hii kada mhumimu ili wawe na uelewa mkubwa katika kujikinga wao wenyewe, lakini pia kuwahudumia wagonjwa na washukiwa wa. covid 19 katika halmashauri zao," amesema Msenza.

Dk. Daniel Mzee akiongea kwa niaba ya Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, amesema kuwa mkoa wa Shinyanga umejipanga kikamilifu katika kupambana na janga la virusi vya corona kwa kuendelea kuwajengea uwezo wataalam wa afya.

Awali akifunga mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, licha ya kutoa pongezi kwa wadau hao amewataka wataalam hao kwenda kutekeleza majukumu ya kitaalam katika kupambana na virusi vya Covid -19, bila kuweka hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo.

Jumla ya wataalam wa afya 55 wa kada ya udaktari, wauguzi, Wataalam wa maabara, usafi na wanaohusika na huduma katika gari la wagonjwa, kutoka katika halmashauri ya mji wa Kahama, Ushetu,na Msalala wamepewa mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu.

Chanzo: --