Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiwasi watanda ukosefu wa dawa za 'antibiotic'

Antibiotic Upoungufu.png Wasiwasi watanda ukosefu wa dawa za 'antibiotic'

Wed, 25 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa wa Afya wa Kamisheni ya Ulaya wamelazimisha kuitisha mkutano kufuatia nchi za bara hilo kukumbwa na ukosefu wa dawa aina ya antibiotic.

Nchi za Ulaya ambazo zinaendelea kutatizwa na ugonjwa wa Uviko-19 na magonjwa mengine katika msimu huu wa baridi kali hivi sasa zinakabilwia na ukosefu mkubwa wa dawa khususan zile za antibiotioc kutokana na kuwa nchi hizo zimekuwa zikitegemea sana kununua mahitaji ya dawa muhimu kutoka China na kufuatia vita vinavyoendelea sasa huko Ukraine.

Makundi ya watumiaji na wataalam wa afya ya umma wametoa wito kwa wadhibiti wa sekta ya madawa katika eneo la Ulaya kuchukua hatua za zaidi ili kukidhi mahitaji ya dawa ya amoxicillin na matumizi ya antibiotic nyingine ili kutibu maambukizo ya bakteria.

imeelezwa kuwa, siku hizi wagonjwa wengi wamekuwau wakiandikiwa na madaktari kutumia dawa aina ya antibiotic kufuatia kuongezeka magonjwa yanayosababisha matatizo ya kupumua na kuwepo maambukizi ya corona.

Dawa ya amoxicillin na antibiotic nyingine kwa ajili ya kuwatibu watoto zimekuwa adimu barani Ulaya tangu mwezi Oktoba mwaka jana. Kutoweka akiba ya kutosha ya dawa na kutojiandaa taasisi za afya barani Ulaya kwa ajili yakukabiliana na mamabukizi ya magonjwa ya msimu na corona ni moja ya sababu iliyopelekea kushuhdia uhaba wa dawa katika nchi za Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live