Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiwasi uchangia matatizo ya Akili kwa 35.8%, pombe 7.6 %

Depression Symptoms Signs Prevention Treatment Anxiety Mental Disorder Infographic Depress Character Sonona inachangia matatizo ya Akili kwa 35.8%, pombe 7.6 %

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: MillardAyo

Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili ya Mirembe imetoa taarifa ya uchunguzi uliofanyika katika banda la Hospitali hiyo kwenye Dodoma Festival .

Taarifa imesema ———"Ili kupima na kutambua uwepo wa dalili za magonjwa ya akili, watu waliotembelea Banda la Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, nyenzo mbalimbali zilitumika, zikiwemo PHQ-9 kwa uchunguzi wa sonona, GAD-7 kwa uchunguzi wa ugonjwa wa wasiwasi, pamoja na AUDIT kwa kutathmini matumizi mabaya ya pombe.

"Takwimu zilionyesha kwamba kati ya Wananchi 92 waliotembelea banda la Hospitali ya Mirembe, Wananchi 22 (23.9%) waligundulika kuwa na tatizo la wasiwasi na kati yao Wananchi 8 (8.7%) waligundulika kuwa na tatizo la wasiwasi mkubwa"

"Wananchi 33 (35.8%) waligundulika na tatizo la sonona, kati yao Wananchi 5 (5.4%) waligundulika na tatizo la Sonona kali, vilevile Wananchi 7 (7.6 %) waligundulika na tatizo la matumizi mabaya ya pombe, na kati yao Watu 4 (4.3%) waligundulika na dalili za uraibu wa pombe"

"Watu wote waliogundulika kuwa na matatizo ya afya ya akili walishauriwa na kupewa rufaa ya kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kuanzishiwa matibabu endapo watakua wamekidhi vigezo"

Chanzo: MillardAyo