Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiotumia ARV's kusakwa!

ARV's Wasiotumia ARV's kusakwa!

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids) Dk Leonard Maboko amesema kati ya watu takribani milioni 1.7 wanaoishi na virusi vya Ukimwi nchini, wanaotumia dawa ni milioni 1.5 pekee.

Dk Maboko aliyasema hayo mjini Moshi wakati wa hafla ya kuchagia mfuko wa VVU na Ukimwi, iliyoandaliwa na kampuni ya Geita Gold Mine Limited(GGML) kwa kushirikiana na Tacaids kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili kupambana na kudhibiti ugonjwa huo hapa nchini.

Aidha Dk Maboko aliwataka wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali kushirikiana pamoja ili waweze kupambana na kupunguza maambukizi ya Ukimwi nchini kwa kuwa jambo hilo linamgusa kila mwanajamii.

"Tunaomba sana watu waweze kuliitikia na kulifahamu hili jambo kwamba ni la kwetu sote, hakuna Mtanzania ambaye anaweza kusema hajawahi kupata athari za Ukimwi katika familia, wengi wetu sasa hivi tumeshapatwa na hili jambo,” amesema.

Aitha Mkurugenzi huyo anaamini kuwa wafanyakazi katika makampuni, mashirika ya umma na watu binafsi, bado ni nguvu kazi na inatakiwa hivyo ni wajibu wa kil mmoja kuhusika katika kuilinda kada hii na ndiyo maana mapambano dhidi ya ukimwi yanatakiwa kufanyika kwa umoja.

"Kazi bado tunayo ya kufanya hata kama tumepunguza vifo vitokanavyo nan a janga hili kwa miaka 10 iliyopita, hata hivyo, kama nchi bado tunasuasua sana watu kupima ndiyo maana katika watu wanaodhaniwa kuwa kuishi ni virusi hivyo ni 1.7 milioni. Na ni watu 1.5 milioni ndiyo wanatumia dawa,"alisema Dk Maboko

Aliongeza kusema kuwa: “Kuwatafuta watu 200,000 sio kazi ndogo, zamani tulikuwa tunapima watu wote, sasa hivi unaambiwa unatakiwa uwe na 'targeted tasting' kwa sababu unapotoa vitendea kazi vingi kwa ajili ya kupima kumpata mtu mmoja inaonekana kama ni hasara fulani, maana unatumia nguvu sana kumpata huyu mtu mmoja,"

"Ndio maana leo unaweza kuzungumzia 'index tasting' kwamba mtu anayekuja kwenye kliniki akapimwa anaambiwa alete wenzi wake kwasababu kuna uwezekano mkubwa wale wenzi wake na wenyewe wakaweza kuwa na virusi vya ukimwi, sasa hizo ni jitihada za kupunguza," amesema.

Naye Makamu wa Rais wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu Geita (GGML), Simon Shayo amesema kwa kushirikiana na serikali bado juhudi za kupambana na maambukizi mapya ya Ukimwi zinaendelea na kwamba wamefanikiwa kukusanya kati ya Sh1 bilioni na Sh1.5 bilioni kila mwaka.

"Tunafahamu ndani ya nchi yetu kuna makundi ambayo bado yapo hatarini lakini kwa bahati mbaya makundi yanayotarajiwa kwa mustakabadhi wa nchi yetu hasa ni vijana ambao ni makundi yanayoongoza kwenye maambukizi,"

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema maambukizi ya Ukimwi hapa nchini yanapoteza nguvu kazi ya Taifa, hivyo akawataka wadau kuongeza nguvu katika kuchangia mfuko huo ili kupambana na kudhibiti maambukizi mapya ya Ukimwi hapa nchini.

"Taifa linapoteza nguvu kazi ya vijana hapa nchini kutokana na jambo hili, ndugu zangu pamoja na kujivunia mafanikio haya ya kupambana na VVU na Ukimwi bado ni tatizo nchini, takwimu zinaonyesha uwepo wa maambukizi mapya ya VVU hususani kwa makundi maalum wakiwemo vijana,"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live