Dodoma. Kati ya wasichana 100 nchini Tanzania, 27 hujifungua wakiwa na umri chini ya miaka 18.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa takwimu hizo leo Jumanne Novemba 26, 2019 mjini Dodoma katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa wanawake duniani.
Amesema idadi hiyo ni kubwa ingawa Serikali imepanga kuipunguza hadi kufikia watoto 13 Juni 22, 2020.
Waziri huyo amesema mapambano dhidi ya mimba za utotoni bado ni makubwa kutokana na jamii kutokuwa na mwamko licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali.
"Tunataka Juni 22,2019 tuwe na asilimia 13.5 kutoka asilimia 27, lazima tusimamie mila na desturi zetu zinazopinga ukatili wa wanawake tukiwashirikisha wazee na viongozi wa dini katika maeneo yetu," amesema Ummy.
Waziri huyo amewataka viongozi kuiga mfano wa mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ambaye ni kinara wa mapambano ya ndoa za utotoni kwa kauli mbiu yake ya ‘sukuma ndani’.