Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasafiri kupimwa Ebola kwa Magufuli

Who Kuanza Kutoa Chanjo Ya Ebola Wasafiri kupimwa Ebola kwa Magufuli

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeweka kituo maalum cha ufuatiliaji wa ugonjwa wa Ebola kwa abiria wanaotoka mikoa ya mipakani mwa Tanzania na nchi jirani  katika kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa huduma za maabara kutoka Manispaa ya Ubungo Nalimi Nacharo, amesema kituo hicho kitatumika kuwapima ugonjwa wa Ebola abiria wanaoingia nchini kutokea mikoa ambayo tayari serikali imetangaza kwamba ipo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.

Kwa upande wake Meneja wa kituo hicho Isihaka Waziri, amesema tayari wameshawaelimisha madereva wa mabasi yanayotoka katika mikoa hiyo kuhakikisha wanapoingia kituini hapo wasishushe abiria mpaka wafike kwenye kituo cha upimaji Ili waweze kupimwa ugonjwa wa ebola

Nao mawakala wa mabasi kutoka nchi za Uganda ambako ndiko ugonjwa huo upo na wale ambao mabasi yao yanatokea maeneo ya mipakani mwa nchi Faraji Musa na Mohamedi Hassan wamesema hatua hiyo ya serikali itasaidia kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini na kushauri kuwekwa kwa vituo kama hivyo kwenye maeneo mengine ya vituo vikuu vya mabasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live