Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapimwa homa ya ini bure Muhimbili

Ini Wapimwa.png Wapimwa homa ya ini bure Muhimbili

Sat, 29 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili leo Julai 28, 2023 imetoa huduma ya vipimo vya ugonjwa wa homa ya ini bure, ambapo matarajio ilikuwa kupima watu 500.

Akizungumza hospitali hapo ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani, Dk Eva Wiso wa Hospitali ya Muhimbili, ambaye ni bingwa wa magonjwa ya mfumo wa chakula na magonjwa ya ini, amesema takwimu zinaonesha watu zaidi ya million 250 duniani kote wanaishi na virusi vya homa ya ini.

Amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kuongezewa damu isiyo salaa, vitu vyenye ncha kali na pia ngono isiyo salama.

Siku ya Homa ya Ini Duniani huadhimishwa Julai 28, ikiwa na lengo la kutoa elimu na hamasa kuhusu ugonjwa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live