Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waombwa kujiunga kwa wingi NHIF      

085148544e8344335e43d4daba837667 Waombwa kujiunga kwa wingi NHIF      

Tue, 23 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKAZI wa Mwanza wameombwa kujiunga na huduma za matibabu zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ili waweze kunufaika na huduma za tiba zinazotolewa na mfuko huo.

Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki jijini hapa na Kaimu Katibu Tawala ( Rasilimaliwatu) Tutubi Mangazeni alipokuwa akifungua warsha ya siku moja kwa viongozi na wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE).

Alisema kwa sasa huduma zinazotolewa na mfuko kupitia kwa watoa huduma wake, zimeboreshwa zaidi na za kisasa .

"Kwa sasa kuna magonjwa mengi yanayoibuka ambayo kama mtu hajajiunga kwenye mfuko itakuwa taabu kubwa,"alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Mwanza, Aloysius Mapembe alisema wamenufaika na warsha hiyo ya siku moja kwa kuwa wamepata fursa ya kujifunza kwa kina na kufahamu huduma zinazotolewa na NHIF.

Kwa upande wake, Meneja wa NHIF Mkoa wa Mwanza, Jarlath Mshashu alisema lengo la warsha hiyo ya siku moja kwa viongozi hao wa vyama vya wafanyakazi ni kuwapatia elimu juu ya huduma zinazotolewa na mfuko ili wawe mabalozi wazuri kwenye sehemu za kazi.

Chanzo: habarileo.co.tz