Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waogopa kutumia kondomu za kike, wataja sababu

Uhaba Kenya Kondomu Waogopa kutumia kondomu za kike, wataja sababu

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalamu wa afya Wilaya ya Ileje mkoani hapa, wameagizwa kuanza kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kondomu za kike ili kukabiliana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na Ukimwi.

Agizo hilo limetolewa leo Januari 30, 2024 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili katika Halmashauri ya Ileje baada ya kuibuka kwa hoja ya wanawake wilayani humo, kuogopa kutumia kondomu kutokana na ukubwa wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Ukimwi ambaye ni Diwani wa Kata ya Itale, Fahari Mwampashi amesema hofu ya watumiaji wa kondomu hizo, wamesema kubwa ukilinganisha na maumbile yao wakitaka zipunguzwe.

“Wanawake wanaogopa kuvaa hizo kondomu wakidai zitabakia ndani na kuhatarisha afya zao, huku wakiomba wataalamu wa afya kupitia ofisi ya mganga mkuu kuwekeza nguvu ya utoaji elimu," amesema Mwampashi.

Kwa upande wake Diwani Viti maalumu, Vema Rungwe amesema matumizi ya kondomu za kike yana changamoto za ukubwa na pia hazitangazwi kwa jamii, ili kuleta uelewa kama inavyofanywa kwa kondomu za kiume.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ubatizo Songa amewataka wataalamu wa afya wilayani humo, kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kondomu za kike na kiume ili jamii iwe na uelewa wa kutosha.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo, Joyce Ongati amekiri kuwepo kwa changamoto ya matumizi ya kondomu za kike, licha ya elimu kutolewa na kuahidi kuendelea kuongeza juhudi za kutoa elimu zaidi.

Mmoja wa mwananchi aliyezungumza na Mwananchi, Mariamu Shimwela amesema awali waliletewa kondomu hizo, lakini wanaogopa kuzitumia kwa hofu ya maumbile yao kuwa madogo wakilinganisha na ukubwa wa kondomu zilivyotengenezwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live