Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wanusurika kifo ajalini, akiwamo DC wa Newala

44688 Pic+ajali Wanne wanusurika kifo ajalini, akiwamo DC wa Newala

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo na watu wengine watatu wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kupata ajali na kupinduka.

Tukio limetokea eneo la Mandawa jana saa mbili usiku wilayani  Kilwa Mkoa wa Lindi  wakati mkuu huyo akiwa safarini kwenda Dar es Salaam.

Jasiri Nguru, mmoja wa majeruhi amesema ajali hiyo imetokea saa 2.30 usiku Kijiji cha Mandawa Kilwa baada ya gari hiyo kuyumba.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine, Muhaji Mohamedi  amesema amepokea majeruhi wanne  ambao ni Aziza Mangosongo, Mwanahamisi  Naenda, mkazi wa Kitangali, Zaituni Lipau  na Jasiri Nguru.

Amesema wanatarajia kuwapa rufaa majeruhi kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kwa matibabu  zaidi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatus Chalya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema dereva Daudi  Kakulilo wa gari hilo la Serikali anashikiriwa  na polisi kwa mahojiano.



Chanzo: mwananchi.co.tz