Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake wenye waume hawa hatarini

45540 Pic+hatarini Wanawake wenye waume hawa hatarini

Sat, 9 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam: Wanawake walioolewa na wanaume wanaovuta sigara, wanywaji wa pombe kali, na walio katika kikomo cha hedhi wapo katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watu wazima kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dk Delilah Kimambo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake kwa lengo la kuhamasisha mazoea ya upimaji afya, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani leo.

Alisema tafiti za hivi karibuni zimeonyesha magonjwa ya moyo na kiharusi yanasababisha vifo kwa wanawake wengi duniani, ambapo mwanamke mmoja katika kila watatu anakufa kwa magonjwa hayo na asilimia 90 wanaviashiria hatarishi vya kuugua.

“Mwanamke anayeishi kwa muda mrefu na mwanaume anayevuta sigara anaweza kupata madhara ya moyo kupitia moshi wa sigara anayovuta mume wake,” alisema.

Dk Delilah alisema mbali na moshi wa sigara, pia mwanamke anapofiki kikomo cha hedhi anakuwa kwenye hatari kupata magonjwa ya moyo.

Mwananchi ilizungumza na baadhi ya wanawake waliofika kupima magonjwa ya moyo ili kujua kama wanaufahamu na viashiria vya ugonjwa hayo, wengi walisema hawajui.



Chanzo: mwananchi.co.tz