Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake waonywa matumizi ya P2 kiholela

P2 Wabunge (600 X 357) Wanawake waonywa matumizi ya P2 kiholela

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Edgar Mahundi amewaonya wanawake nchini kuacha kutumia vidonge vya kuzuia mimba baada ya tendo la ndoa maarufu kama P2 kwa kuwa vidonge hivyo vinaweza kuwasababishia ugumba kwa sababu vinatumika bila maelekezo kutoka kwa daktari

Edgar Mahundi ameyasema hauyo wakati anatoa taarifa ya operesheni waliyoifanya Kanda ya ziwa na kuzikuta Dawa hizo zikiuzwa kiholela bila maelekezo ya Daktari.

"Mabinti wengi wamekuwa wakizikimbilia hizi dawa, hizi dawa maarufu zinaitwa P2, sasa P2 ni aina fulani ya homoni ambazo zinazalishwa mwilini, sasa unapotumka hii dawa maana yake unaenda kuvuruga ule utaratibu mzima wa uzalishaji wa homoni husika au vichocheo husika kwenye mwili mwisho wa siku Sasa anapohitajika binti apate ujauzito kwa sababu ametumia hii dawa bila utaratibu  hapati tena ujauzito mwisho wa siku tunakuwa na watu ambao wanashindwa kupata watoto", alisema Mahundi

Aidha Mahundi anasema vijana wa kiume pia wapo hatarini kwa sababu wamekuwa wakitumia dawa feki za kuongeza nguvu za Kiume kwa ajili ya tendo la ndoa.

" Wanatumia hizi dawa kuongeza nguvu za kiume, dawa hizi tumezikuta kwenye maduka binafsi ya dawa zinaitwa Vega100, na dawa hizi zenyewe hazijasajiliwa lakini pia tumefatilia  kiwanda kilichoandikwa hapo hakipo duniani kwahiyo moja kwa moja dawa hii nayo ni bandio", alisema Mahundi.

Baadhi ya wananchi wamewaomba vijana kuacha kutumia dawa bila maelekezo kwa ajili ya usalama wa Afya zao.

"Nawashauri vijana wetu au waakina mama wote wanaotumia dawa za kuzuia uzazi au kuzuia mimba ni bora tutumie kinga kukiko kutumia dawa kwa sababu dawa zinaenda kuharibu mfumo wao wa uzazi, kwahiyo ni afadhali mtu atumi kinga ajikinge Ile mimba isipate kutungwa kuliko kutumia dawa, kwahiyo ushauri wangu hasahasa kwa vijana au kwa wadada na wamama wasitumie dawa either watumie kinga kuliko Dawa za kuzuia uzazi", alisema Khamis.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live