Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake waongoza kwa magonjwa ya ngono

Batch Maxresdefault 22 Wanawake waongoza kwa magonjwa ya ngono

Sat, 30 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Ukimwi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, imesema kuwa katika Wilaya hiyo takwimu zinaonyesha uwepo wa idadi kubwa ya Wanawake walioambukizwa Magonjwa ya Ngono kuliko wanaume.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Diwani, Christopher Ndamo akiwasilisha Taarifa ya kamati yake kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo jana amesema jumla ya Wanawake 226 wamepata Magonjwa hayo huku wanaume wakiwa 75.

Amesema kuwa sababu za Wanawake wengi kupata Magonjwa hayo inatokana na uwepo wa Biashara ya Ngono kwenye Wilaya hiyo lakini pia wajawazito wamekuwa na tabia ya kwenda Kliniki bila ya wenza wao.

Amesema kuwa mbali na wengine kupata Magonjwa hayo kupitia biashara ya Ngono, lakini wengine wamepata wakiwa wajawazito kutokana kushindwa kwenda Kliniki na wenza wao ili wapatiwe Elimu ya jinsi ya kujinga na Magonjwa hayo.

”Lakini pia tumegundua kamati za UKIMWI ngazi ya vijiji na kata hazifanyi kazi, hivyo tumeomba Baraza lituongezee Muda wa ziara ili tutembelee vijiji na kata zote kwa ajili ya kuweza kufufua kamati hizi ili ziweze kutoa Elimu kwa wananchi jinsi ya kujikinga na Magonjwa haya pamoja na UKIMWI,” Amesema Ndamo.

Aidha amesema kuwa kamati hiyo imewaomba Madiwani kuhamasisha jamii kutumia Kondomu Kama Kinga muhimu ya Magonjwa hayo pamoja na UKIMWI mwenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live