Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake wanaotumia vidonge kuongeza hamu ya ngono, Hatarini kupata saratani

Ngono Idadi ya magonjwa ya saratani inaongezeka duniani

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake wameshauriwa kuacha kuweka dawa za kuongeza hamu ya ngono ambazo hazijapimwa na wataalamu katika sehemu zao za siri, kwa kuwa kufanya hivyo kunawaweka hatarini kupata Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Mtaalamu na Mshauri wa Afya ya Umma, Jinsia na Maendeleo ya Jamii, Dkt. Katanta Simwanza amesema takwimu za mwaka 2021 za Saratani katika Hospitali ya Ocean Road zinaonesha aina ya Saratani zinayowapata Wanawake wengi ni Saratani ya Shingo ya Kizazi (43%), Saratani ya Matiti (14.2%) na Saratani ya Koo (3.8%).

Ametaja utumiaji wa dawa za kusisimua mwili ambazo hazijapimwa, ngono zisizo salama, kushiriki tendo la ndoa mapema, kujamiiana na wanaume wasiotahiriwa, matumizi ya virutubisho kama potasiamu ili kuongeza hamu ya ngono vinaweza kuwa chanzo, cha Saratani hizo na pia vinaweza kusababisha kuondolewa kwa harufu ya asili ukeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live