Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake 333,000 hupatwa na tatizo la uzazi kila mwaka

25737 WANAWAKE+PIC TanzaniaWeb

Wed, 7 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kati ya wanawake 2.2 milioni wanaobeba ujauzito kila mwaka hapa nchini, asilimia 15 ambayo ni sawa na 333,000 wanapata matatizo mbalimbali yatokanayo na uzazi.

Hayo yamesemwa leo, Jumanne Novemba 6, 2018, jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya ‘Jiongeze! Tuwavushe Salama’ inayolenga kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga.

Ummy amesema ili kuondokana na tatizo hilo, ni lazima kila mkuu wa mkoa ale kiapo kuhakikisha akitoka kwenye uzinduzi huo atakuwa na uwezo wa kuweka mbinu za kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi chini ya idara za kinga.

“Kwa mujibu takwimu za afya 2017, wajawazito 2.2 milioni wanaobeba ujauzito nchini kila mwaka, asilimia 85 yao hujifungua bila shida,” amesema Ummy.

Amesema, “Ni asilimia 15 hupata matatizo wakati wa ujauzito, uchungu, wakati wa kujifungua na mpaka wiki sita baada ya kujifungua takriban (wajawazito) 333,000.”

Waziri huyo amesema matatizo mengi ya wajawazito huja bila matarajio, lakini yanazuilika na kutibika kama mama atahudhuria kliniki wakati wa uchungu na hata wiki sita baada ya kujifungua .

Amesema sababu za vifo zinajulikana kwani wajawazito wengine hufariki baada ya kutokwa na damu nyingi.

“Hali halisi ya huduma za afya, asilimia 24 kila wanawake 100 wanahudhuria kliniki chini ya miezi mitatu ya ujauzito wao, wanawake 86 hawaendi kliniki ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya ujauzito wao,” amesema.

Ameongeza kuwa, “Wanaohudhuria kliniki ni asilimia 51 na wale wanaojifungulia kwenye vituo ni asilimia 63 pekee.”

Chanzo: mwananchi.co.tz