Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake 12,500 wafaidika na mradi wa kupunguza vifo

7508fee147526e28d06c97ad27b6b4d9 Wanawake 12,500 wafaidika na mradi wa kupunguza vifo

Sat, 24 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WANAWAKE 12,500, mkoani Manyara wameweza kunufaika na mradi wa Momcare unaotekelezwa na shirika la PharmAcess unaolenga kuwakomboa mama na mtoto ili kupunguza vifo vya wanawake na watoto.

Mratibu wa Mradi wa MomCare, Liberatha Shija alisema hayo alipokuwa kwenye uzinduzi wa jengo la mama na mtoto lililogharimu Sh milioni 23 katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Babati.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa safari ya mama mjamzito pamoja na changamoto anazokutana nazo baada ya kujifungua shirika la hilo limeona umuhimu kushirikiana na serikali katika harakati za kupunguza magonjwa ya kinamama na vifo vinavyotokana na uzazi na kuboresha taaluma na matumizi ya data wanazozikusanya katika vituo vya kutolea huduma ikiwa ni pamoja na kuongeza huduma mbalimbali zinazotolewa katika vituo.

Liberatha alisema katika miaka yote hiyo wamekuwa wakiongeza vituo kwa awamu na mwaka 2019 walikuwa na vituo nane, kati ya hivyo vitano ni vya mkoa wa Manyara na vitatu ni vya mkoa wa Kilimanjaro na mwaka wa pili waliongeza vituo 15 na mpaka sasa tayari wameongeza vituo vingine 25 ambavyo vinafanya kukamilika kwa vituo 40.

Kati ya vituo 40 vinavyotekeleza mradi wa Momcare chini ya shirika la Pharmacess, vituo 37 vipo mkoa wa Manyara na vituo vitatu vipo mkoa wa Kilimanjaro na shirika limeweza kukarabati miundombinu mbalimbali pale inapobidi ikiwa ni pamoja na kuvipatia vifaa tiba pamoja na dawa muhimu zinasaidia katika uzazi.

“Tumechangia mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (ICHF) kwa kiwango cha Sh milioni 300, mpaka sasa tunaendelea kuboresha sehemu mbalimbali na huduma zile za mama na mtoto tunajitahidi kuhakikisha zinapatikana kulingana na miongozo ya Wizara ya Afya na miongozo ya Shirika la Afya Duniani,” aliongeza .

Magreth Isaya ambaye ni mtoa huduma kwa mama na mtoto alisema kuwa awali kabla ya kuboreshewa jengo la mama na mtoto kulikuwa hakuna usiri kwa wateja wao kwani baadhi ya vyumba vilikuwa wazi kwa juu pamoja na milango kutofunga .

Katibu Tawala wa wilaya ya Babati, Halfani Matipula alisema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa shirika hilo pale watakapohitaji msaada ili waweze kufanikisha miradi yao ambayo imekuwa msaada kwa wanawake wa wilaya hiyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz