Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume watatu walazwa wodi ya Kipindupindu kwa kunywa dawa ya nguvu za kiume

2015 147 660x400

Sun, 28 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Wanaume watatu wakazi wa kijiji cha Katete nchini Zambia wamezua mshangao kwa watu baada ya kupelekwa kwenye Kituo cha wagonjwa wa Kipindupindu wakiwa wamezidiwa kwa kuumwa wakihofiwa kuwa na Kipindupindu.

Baada ya kufanyiwa vipimo, majibu yalionesha kuwa tofauti na ilivyofikiriwa, wanaume hawa walikuwa wamekunywa dawa ya kuongeza nguvu za kiume katika tendo la ndoa ijulikanayo kama Mvubwe.

Ripoti ya madaktari wa hospitali hiyo ya kipindupindi walieleza kuwa vipimo vinaonesha kuwa mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa hiyo, ulisababisha mchafuko tumboni hivyo ikahusishwa na Kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu katika tendo la ndoa.

BREAKING: Tido Mhando alivyofikishwa Mahakamani leo



TRL inapoteza zaidi ya Mil.200 kwa siku kutokana na treni kutofanya kazi.

Chanzo: millardayo.com