Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume waondolewa hofu juu ya chanjo ya COVID-19 kupunguza nguvu za kiume

Ae23b3833341097a447798021df436a6 Chanjo ya Corona

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WANAUME wametakiwa kuacha mawazo kuwa chanjo ya virusi vya corona ya Johnson & Johnson (JJ) kuwa inaua nguvu za kiume, badala yake ni muhimu kuchanja ili kuondokana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

Aidha kuna tabia ya baadhi ya watu kuchanja chanjo ya JJ kimya kimya kisha kuwapotosha wenzao vijiweni na maeneo mbalimbali kuwa chanjo hiyo haifai ilihali imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO)na ndio maana wananchi wanachanja.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk Sylvia Mamkwe alisema chanjo hiyo haina uhusiano wowote na kuua nguvu za kiume.

Alisema chanjo ya JJ ni salama na ndio maana Tanzania imeileta kwani inahimili joto la Tanzania na haina uhusiano wa kuua nguvu za kiume kama watu wanavyodai.

"Chanjo hii ukishachoma inaleta ujumbe yaani unaweza kujisikia kuchoka au dalili nyingine lakini haiui nguvu za kiume, acheni maneno potofu, wanaume nendeni mkachanje chanjo,"alisema.

Alisema endapo mwanaume akiwa kichwani hayupo sawa hawezi kujisikia hamu ya tendo la ndoa sababu ya changamoto za maisha au la lakini si kudai kuwa chanjo hiyo inaua nguvu za kiume.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live