Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume wanaovaa suruali zaidi ya 'size' 40, mwanamke 35, afya yako ipo hatarini

Janabipic Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi huyo Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Prof. Mohamed Janabi amesema Watu wenye uzito mkubwa wanapaswa kuchukua hatua za haraka kupunguza miili kabla hawajaingia kwenye hatari ya Magonjwa Yasiyoambukiza

Amesema kasi ya ongezeko la Wagonjwa wa Figo na Kisukari inaonesha wazi Watu wengi wana mtindo wa Maisha usiofaa ikiwemo ulaji mbaya wa Vyakula, Matumizi makubwa ya Pombe na Dawa za Kutuliza Maumivu bila utaratibu mzuri pia kutofanya mazoezi

Ameongeza kuwa tafiti zinaonesha 90% ya Watu hawajui kama Figo zao zina matatizo huku 40% wakifika Hospitali wakati Ugonjwa ukiwa hatua ngumu na za mwisho kutibika na hauwezi hata kusafisha Damu (Dialysis)

Kwa mujibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) ili kuepuka Magonjwa yanayotokana na Vyakula, Watu wanapasawa kutotumia Vyakula Vilivyopikwa kwa Mafuta Mengi, Vinywaji Venye Sukari Nyingi zikiwemo Soda aina zote na Juisi za Viwandani

Chanzo: www.tanzaniaweb.live