Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume wamiminika Muhimbili kupima tezi dume

9461 Tezi+pic.png TZWeb

Mon, 18 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Idadi ya wanaume wanaokwenda kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya tezi dume imeongezeka kutokana na wanaume wengi kuwa na hofu ya kupata maradhi hayo.

Hayo yameelezwa leo Juni 18 na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya mfumo wa mkojo na tezi dume, Isack Mlatie wakati wa maonyesho ya huduma zinazotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Soma Zaidi: Makonda kupima tezi dume nyumba kwa nyumba

Dk Mlatie amesema kumekuwepo na mwamko mkubwa wa wanaume kufahamu kuhusu ugonjwa huo.

Amesema kwa sasa idara hiyo inapokea zaidi ya watu 100 kwa wiki tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

"Huu ugonjwa ulikuwepo muda mrefu ila uelewa ndio umeanza kuonekana miaka ya karibuni nadhani kwa sababu hata matibabu yanapatikana na utaalam umeongezeka,"amesema na kuongeza:

"Sasa hivi hata wasio wagonjwa wanakuja wengi wao tunabaini wanakuwa na hofu kutokana na ugonjwa huu unavyozungumzwa kwenye jamii," anasema.

Soma Zaidi: Wanaume watofautiana kampeni ya Makonda upimaji saratani ya tezi dume nyumba kwa nyumba

Maonyesho ya huduma zinatolewa MNH yamezinduliwa leo na yatafanyika kwa siku tatu yakitoa fursa kwa watu kupima afya zao bure.

Chanzo: mwananchi.co.tz