Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume waitwa kupima tezi dume

PSA TEST Awali vipimo vya kidole vilikimbiwa na wanaume wengi

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalamu wa afya wamewataka wanaume kuwahi mapema kupima saratani ya tezi dume kwa kuwa kipimo kilichokuwa kikifanyika kwa njia ya kidole kwa sasa hakitumiki tena kutokana na kukua kwa teknolojia.

Na sasa kipimo kinachotumika sasa ni kile cha damu ambayo huchunguzwa protini maalum ya tezidume (PSA) na kipimo cha kuchunguza ukubwa na umbo la tezidume, hufanyika kama vipimo vya awali.

Hayo yamesemwa Alhamisi, Machi 17 2022 na Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Caroline Swai alipokuwa akiutambulisha mradi wa kupambana na saratani (TCCP) kwa vyombo vya habari

Chanzo: www.tanzaniaweb.live