Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume waaswa kupima saratani ya matiti

94702 Saratani+pic Wanaume waaswa kupima saratani ya matiti

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Tanzania (KIUT) pamoja na Maabara ya Lancet Tanzania wametoa elimu na huduma ya vipimo vya saratani ya matiti katika hafla ya maadhimisho ya siku ya saratani ya matiti duniani.

Hafla hiyo iliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam, ilihudhuriwa na zaidi ya watu 200 waliopewa elimu juu ya saratani hiyo na kufundishwa namna ya kujipima wenyewe kwa kutumia teknolojia ya FNAC ili kubaini kama wana saratani au la.

Vipimo vya kujichunguza saratani ya matiti vilifanywa na madaktari wote kutoka maabara ya KIUT na Lancet.

Mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka chuoni hapo, Dk Shaila Shah alieleza kwamba saratani ya matiti haiwapati wanawake pekee, hivyo, wanaume pia ni muhimu kujipima ili kubaini kama wana saratani hiyo.

Aliwafundisha namna ya kujipima saratani hiyo kwa kutafuta uvimbe kuzunguka eneo la titi lote. Aliwaeleza jinsi ya kujitambua na kutumia takwimu vizuri na kuepuka tabia hatarishi za saratani hiyo.

Maabara ya Lancet Tanzania imejiandaa kufanya upimaji wa magonjwa ya aina nyingi ikiongozwa na wataalamu zaidi ya 90 wa magonjwa ya akili.

Pia Soma

Advertisement
Aina hiyo ya saratani kwa sasa inatajwa kushika nafasi ya pili miongoni mwa aina za saratani.

Chanzo: mwananchi.co.tz