Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume kushuhudia wake zao wakijifungua

Kujifungua Pic Data Wanaume kushuhudia wake zao wakijifungua

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanaume waliokuwa wakitamani kuwasindikiza wake zao wakati wa kujifungua sasa watapata fursa hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure.

Fursa hiyo imekuja baada ya Serikali kujenga jengo la huduma za afya ya mama na mtoto ambalo litakuwa na vyumba 10 maalum kwa ajili ya wenza watakaopenda kusindikizana wakati wa kujifungua.

Akitoa taarifa fupi ya jengo hilo kwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango wakati wa kulizindua leo Jumanne, Septemba 13, 2022, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Bahati Msaki amesma mbali na jengo hilo kuwa na vyumba viwili za wanawake kujifungulia lakini pia lina vyumba maalum (private) vya kujifungulia.

“Kuna vyumba vya private kwa ajili ya kina mama wanaotaka kujifungua kwa usiri na wanaotaka kuingia na waume zao na ndugu zao, kwahiyo mama akija tunampatia chumba na anajifungua mume wake akiwepo,” amesema Dk Bahati

Jengo hilo lililojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) lenye ghorofa tano zenye sakafu (floor) sita lina uwezo wa kubeba vitanda 261.

Naye Dk Mpango amewapongeza TBA kwa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa wakati huku akiwataka viongozi na wataalamu kuwahimiza kina baba kuhudhuria kliniki ili kupata mtoto mwenye afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live