Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume kupimwa VVU, TB baa

6956 NDUGULILE BUNGENI.jpeg TZW

Mon, 23 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imeweka mikakati ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Kifua Kikuu (TB) ikiwemo kampeni ya kuwapima wanaume kwenye baa na vilabu vya pombe.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile ameeleza hayo bungeni leo, mjini Dodoma.

Ameyasema hayo wakati anajibu swali la Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salim aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kukabiliana na maambukizi hayo.

Dk Ndugulile amewaeleza wabunge kuwa wasishangae kuona wataalam wa afya wakipita maeneo hayo ya starehe kwa lengo la kuwapima TB na VVU, ikiwa ni mkakati mahususi kwa ajili ya kuwafikia wanaume wengi.

Akielezea mikakati na hatua zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na maambukizi hayo, Naibu Waziri amesema ni pamoja na kuingiza teknolojia mpya ya upimaji na ugunduzi wa haraka na uhakika wa vimelea vya TB.

“Hadi sasa mashine 97 zimeshafungwa katika hospitali za mikoa na baadhi ya halmashauri na mashine nyingine 90 zimeshanunuliwa na zinatarajiwa kufungwa kwenye hospitali za wilaya ambazo zimebakia,” amesema Ndugulile.

Chanzo: habarileo.co.tz