Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume Temeke ruksa kushuhudia wake zao wakati wa kujifungua

Mwanamke Labour Wanaume Temeke ruksa kushuhudia wake zao wakati wa kujifungua

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Rufaa Mkoa Temeke (TRRH) imeanza rasmi kutoa huduma ya kujifungua ukiwa na msaidizi yaani mama, mume, mpenzi au ndugu na kuruhusu mama anayejifungua kuchagua muuguzi anayemtaka kama muongozo mpya wa chati uchungu unavyosema.

Maboresho hayo yamefanywa ili kumwezesha mama mjamzito kupata huduma bora zaidi na kuwa karibu na msaidizi wake pamoja na kuzingatia utu na heshima kwa mama mjamzito.

Hassan Mwauta mkazi wa Chamazi ambaye ni mume wa mmoja wa wajawazito waliotumia huduma hiyo katika hospitali hiyo ameipongeza Serikali kwa maboresho hayo.

“Nilimleta mke wangu kuja kujifungua katika hospitali ya Temeke, nilisikia kuna huduma ya mzazi kujifungua akiwa na mwenza wake na nilipofika nimejionea mwenyewe, nimeshangaa kwa kweli mazingira ni mazuri na huduma ni nzuri, unaweza kuingia na mjamzito wako ukakaa naye muda wowote unaotaka,” amesema Mwauta.

Naye Ofisa Mkunga katika hospitali hiyo, Shukrani William, amesema wodi ya kujifungulia kina mama imeboreshwa na kwamba huo ni moja ya mikakati ya kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha sekta ya afya inaboresha huduma na kuboresha maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live