Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasayansi washauriwa kufanya tafiti zaidi za tiba

Fe8ca7788a07938092725c6f67e83a4d.jpeg Wanasayansi washauriwa kufanya tafiti zaidi za tiba

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANASAYANSI nchini wameombwa kufanya tafiti za kina ili kuliwezesha taifa kujitegemea zaidi katika tiba za aina mbalimbali badala ya kutegemea misaada zaidi kutoka kwa wahisani.

Tafiti hizo zitasaidia upatikanaji wa tiba za aina mbalimbali, ikiwamo dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi ambavyo vimetajwa kushambulia zaidi rika la vijana kuanzia miaka 15 hadi 24.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Daudi Mabula alisema hayo wakati akifungua kongamano la wanasayansi mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani itakayofanyika kitaifa mkoani hapa.

"Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kuwa na miti shamba ya aina mbalimbali, watafiti wetu jikiteni tupate dawa...mtakumbuka virusi vya corona vimetufanya tutumie akili zetu, tukatengeneza barakoa, vifaa vya kujikinga na corona pamoja na sabuni za kunawia mikono,” alisema.

Alisema utegemezi wa wafadhili katika sekta ya afya ikiwemo kutoa misaada ya dawa za Ukimwi ni jambo jema ila halipaswi kuaminika.

Alisema utegemezi wa wahisani katika sekta ya afya ni changamoto kubwa jambo ambalo taifa likiendelea kujikita katika utegemezi huo ipo hatari kubwa katika siku za mbele iwapo wafadhili watajitoa na kuacha kutoa misaada hiyo.

"Serikali itaendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani ili kuanzisha viwanda na kufanyika kwa tafiti ambazo zitatusaidia kupata dawa za maradhi ya aina mbali badala ya kutegemea misaada,"alisema.

Aidha alisema serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya mfuko wa Ukimwi, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi umuhimu wa kuchangia mfuko huo.

Mbali na hilo, pia aliwataka watafiti kuendelea kufanya utafiti wa kubain chanzo halisi kinachoeneza virusi vya corona na kucha tabia ya kukaa ofisini na kusikilizia tafiti za mataifa mengine.

Awali akizungumzia katika mdahalo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya kudhibiti na Kupambana na Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Leonard Maboko alisema time hiyo imejiwekea lengo kwamba ifikapo mwaka 2030 Tanzania kusiwe na maambukizi mapya ya Ukimwi.

"Kwa sasa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa Ile Sera yetu ya tisini tatu kutokana na elimu ambayo tunaendelea kuitoa na ndo maana malengo yetu ni kwamba ifikapo mwaka 2030 tuwe tumetokemeza na kumaliza kabisa maambukizi mapya,"alisema

Chanzo: habarileo.co.tz