Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasayansi Marekani wagundua tiba ya Uviko-19

Tiba Pc Data Wanasayansi Marekani wagundua tiba ya Uviko-19

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Jaribio la wanasayansi kubaini dawa ya homa ya Uviko-19 linaelekea kuzaa matunda baada ya kuwapo kwa taarifa za matumaini makubwa vidonge vya ‘Molnupiravir’ kufanya kazi kwa ufanisi kutibu ugonjwa huo.

Dawa hiyo iliyofanyiwa majaribio na kampuni ya kimataifa ya kutengeneza dawa ya Merck iliyopo nchini Marekani inaweza kuleta suluhu katika kupatikana kwa dawa ya Uviko-19.

Taarifa iliyotolewa na jana na mtandao wa euronews, wagonjwa 775 waliofanyiwa majaribio kupitia dawa hiyo wamepona kikamilifu na sasa kampuni hiyo, inasubiri idhini ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani (FDA) ili ianze kutumika nchini humo.

Kulingana na wanasayansi dawa hii inaweza kupunguza vifo kwa kiwango kikubwa zaidi.

Kampuni hiyo imetengeneza kidonge cha kwanza kinachosemekana kuwa bora dhidi ya virusi hivyo na endapo watapewa idhini dawa hiyo aina ya ‘Molnupiravir’ itakuwa ya kwanza kutibu Uviko-19.

Mwanasayansi Peter Hotez kutoka kampuni hiyo amesema, “Majaribio ya kliniki yanaonyesha kuwa dawa hii ina uwezo wa kufikia idadi kubwa ya watu ikilinganishwa na matibabu ya hivi sasa ya kingamwili ya ambayo hutumiwa kwa kawaida. Katika matumizi dawa hii mgonjwa anapewa kipimo cha vidonge viwili kila siku kwa siku tano.”

Wanasayansi wanasema dawa hiyo ina viwango vya juu vya kuishi kwani hakukuwa na vifo vilivyoripotiwa kwa walioitumia kwenye majaribio ya kliniki.

Kwa mujibu wa mtandao huo, kidonge hicho kinatarajiwa kupatikana nchini Marekani na kitapatikana kote ulimwenguni mwishoni mwa mwaka huu.

Mapema wiki jana, Marekani pia ilianza majaribio ya dawa inayolenga kuwalinda watu wanaoishi na mtu aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa huo kwa watu 2,660 ikiwa ni miezi 13 tangu kupatikana kwa chanjo ya ugonjwa huo.

Chanzo: mwananchidigital