Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaotumia zaidi dawa hii ya maumivu wako hatarini kiafya

Dawa Dawa Wanaotumia zaidi dawa hii ya maumivu wako hatarini kiafya

Sun, 22 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya ya Kenya kupitia Bodi ya Famasia na Sumu (PPB) imeonya kuhusu matumizi mabaya ya dawa maarufu ya kutuliza maumivu nchini humo, Diclofenac.

Katika taarifa ya Bodi hiyo iliyotolewa Ijumaa, Mei 20, bodi hiyo imesema watu wengi wamekuwa wakitumia kupita kiasi dawa hiyo ya Diclofenac, Steroidal Anti-Inflammatory (NSAID) kwa ajili ya kudhibiti maumivu.

Dawa hiyo kwa sasa haishauriwi kutumiwa na wagonjwa wenye historia ya matatizo ya moyo. PBB inasisitiza kuwa Diclofenac ikitumiwa kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu, inahusishwa na ongezeko la hatari ya kuganda kwa damu kwenye mishipa, hasa kwa wagonjwa walio na matatizo ya moyo au hali ya mzunguko wa damu au walio na sababu fulani za hatari ya moyo na mishipa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo watu wanaotumia dozi ya juu ya 150 mg kwa siku na kwa muda mrefu wako katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo na kiharusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live