Dar es Salaam. Wanaotumia vifaa vya mawasiliano ikiwamo kompyuta, simu, tableti wametakiwa kutumia lenzi maalumu ili kujikinga na mionzi inayoathiri macho.
Hayo yamesemwa leo Jumamosi Aprili 6, 2019 na mkurugenzi wa kliniki ya macho ya Karibu Eye Center, Abdillah Dada, kwenye kambi maalumu ya upimaji afya iliyoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
MCL inazalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen, MwanaSpoti na MCL Digital
Dada amesema watoto wa miaka kuanzia mitano hadi 16 ndiyo sana wanaosumbuliwa na tatizo sana la macho kwa siku za hivi karibuni.
Amesema hiyo inatokana na wengi wao kutumia vifaa vya mawasiliano muda mrefu ikiwamo simu, kompyuta bila kuweka vifaa vya kuzuia mionzi.
"Wazazi mtoto akifikisha miaka mitano na kuendelea anajitegemea na anaanza kujifunza au kutumia vifaa hivyo, bila uangalizi hadi atakapoanza kulalamika kuumwa macho au kutoona vizuri ndiyo anakwenda kupimwa.”
Related Content
- Mamia Dar wajitokeza kupima afya bila malipo
- Marumaru zatajwa kusababisha ugonjwa wa miguu, kisigino
- Jitokeze upime afya bure Leaders leo
Dada ameeleza kwenye kliniki yao ya Karibu Eye Center wanaagiza vifaa hivyo kutoka nchini Uturuki vyenye ubora wa hali ya juu.
"Kwenye kambi hii iliyoandaliwa na Mwananchi tunapima macho, tunatoa fremu, tunapokea bima mbalimbali na tunatoa ushauri" amesema Dada na kufafanua kuwa wanatumia mashine za kisasa kutoa huduma ya macho.