Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaojichubua hatarini kupata saratani

Mkorogo (600 X 600) Wanaojichubua hatarini kupata saratani

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tafiti zinaonesha kuwa wanaotumia dawa kubadilisha muonekano wa ngozi (kujichubua), wapo hatarini kupata ugonjwa wa Saratani ya ngozi kutokana na kupigwa na mionzi ya jua.

Daktari Bingwa wa Saratani, Dkt. Hellen Makwani amethibitisha jambo hili na kusema kuwa watu wanaotumia vipodozi vya kujichubua wapo kwenye hatari ya kupata Saratani ya ngozi kutokana na kinga ya ngozi kuondolewa.

"Wanaojichubua wapo kwenye hatari ya kupata saratani ya ngozi kwa sababu mtu huyo anakuwa ameondoa melanin kwenye ngozi yake hivyo mionzi ya jua inaweza kuathiri na kupata ugonjwa," amesema Dkt. Makwani.

Madhara megine ya kujichubua ni pamoja na kupata chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba, Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito, kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika vipodozi, Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)

Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi kuweka mazoea ya kuchunguza afya zao ili kuweza kukabiliana na magonjwa endapo yatabainika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live