Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi watakiwa kupunguza gharama za matibabu

Mon, 15 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Halmashauri ya Jiji la Dodoma imesema iwapo watu watazingatia usafi wa mazingira wataweza kupunguza gharama za matibabu kwa kiasi kikubwa.

Imesema asilimia 70 ya watu wanaofika katika vituo vya afya wanaugua magonjwa yanayosababishwa  na uchafu wa mazingira.

Kauli hiyo imetolea leo Oktoba 13, 2018 na Ofisa Mazingira wa jiji hilo, Ally Mfinanga wakati watumishi wa Hospitali ya Kisasa ya Benjamin Mkapa walipokuwa wakifanya usafi katika Soko Kuu la Majengo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake.

“Mhakikishe mnafanya usafi katika mazingira yenu ili tupunguze mzigo wa gharama za matibabu. Asilimia 70 ya wagonjwa wanaoripoti katika vituo vya afya magonjwa yao yanatokana na uchafu wa mazingira,” amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kisasa ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonce Chandika amesema kwa kufanya usafi, wananchi watawezesha kupunguza gharama za matibabu kwa Serikali.

“Mazingira yakiwa safi ina maana tunapunguza maradhi mbalimbali yanayoletwa na mazingira yaliyo machafu kwa mfano maradhi ya tumbo, kipindupindu na kuharisha na mengine,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz