Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi watahadharishwa kuhusu Ebola

Mollel Vinjiti.png Wananchi watahadharishwa kuhusu Ebola

Sat, 24 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewaasa wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya Ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa kutokea katika nchi jirani ya Uganda.

Dkt. Mollel amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma na kutoa tahadhari hiyo huku akiwataka wananchi kuepuka safari zisizo kuwa za lazima kwenda maeneo ambayo yameripotiwa kutokea ugonjwa huo.

Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya tayari imeshatoa maelekezo kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufanya ufuatiliaji zaidi mipakani kabla ya wananchi kuingia na kutoka nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live