Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi waomba maboresho ya kliniki Muhimbili

4adb41d566acc2bfde966d1cc7c090d8 Wananchi waomba maboresho ya kliniki Muhimbili

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi na wazazi wanaopata huduma kwenye kliniki ya watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemuomba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuongezewa wataalamu wa huduma ya mishipa ya ubongo.

Wananchi hao wameomba yafanyike maboresho kwenye eneo la huduma za vyoo kwa ajili ya kuwasitiri watoto wadogo na kuwekewa feni ili upunguza joto kwa watoto pamoja na kuongezewa mabenchi ya kukalia.

"Mhe tunaomba kuongezwa kwa wataalam wa huduma ya mishipa ya ubongo kwani uhitaji mkubwa" alisema mmoja ya wananchi hao.

Takwimu zinaonesha kitengo cha mishipa ya fahamu na Ubongo, kinahudumia watoto 80 kwa siku, Idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya mabingwa waliopo kwa sasa.

Akijibu maswali ya wananchi na wazazi hao Dk Gwajima alisema ameyapokea maoni na mapendekezo yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi.

"Ndugu zangu nimewasikia, uzuri hapa tupo na Mkurugezi anawasikia pia, lakini kama haitoshi, naomba niwape namba yangu ya kunitumia ujumbe mfupi, hii sio kwa ajili ya kupiga, niandikie ujumbe, tushauri nini tuweze kuboresha, kwa kutumia wataalam wetu tutachukua maoni yenu na tutayafanyia kazi” amesema Dk Gwajima.

Katika hatua nyingine, Waziri amemuelekeza Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyie kazi maboresho ambayo wananchi waliomba kuboreshewa, sambamba nakuendelea kuchukua maoni zaidi kwenye maeneo mbalimbali ambayo yatawasilishwa na wananchi ili huduma ziweze kuboreshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Laurence Museru aliahidi kuyafanyia kazi maboresho hayo, ambayo wananchi waliwasilisha ili kuweza kutatuliwa sambamba na kuongeza wataalam Bingwa wa masuala ya matatizo ya watoto ya Ubongo Pamoja na mishipa ya fahamu.

“Mhe. Waziri tumeyachukua haya ambayo wananchi wamewasilisha mbele yako, lakini mkakati mwingine tulionao ni kuongeza wataalam wabobezi kwa kuwapeleka shule ili wakihitimu waweze kusaidiana na hawa waliopo na kuondoa kabisa mapungufu haya ama kuyapunguza kwa asilimia kubwa. Prof Mseru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live