Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wakumbushwa, ukitelekeza mtoto faini Sh5 milioni au kifungo miezi sita

84451 Pic+ndugulile Wananchi wakumbushwa, ukitelekeza mtoto faini Sh5 milioni au kifungo miezi sita

Fri, 15 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Adhabu kwa mzazi aliyemtelekeza mtoto wake ni faini Sh5 milioni au kifungo kisichopungua miezi 6, Bunge limeelezwa leo Ijumaa Novemba 15, 2019.

Hayo yameelezwa leo bungeni na naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Faida Mohamed Bakari.

Mbunge huyo ametaka kujua ni adhabu gani inatolewa kwa watu wanaotelekeza watoto na kuhoji ni mashauri mangapi yanayohusu wazazi kutelekeza watoto yaliyoripotiwa mwaka 2018/19.

Mbunge huyo amesema adhabu ya Sh5 milioni ni ndogo, akaomba Serikali kupeleka sheria bungeni ili wakaifanyie marekebisho na kuongeza adhabu.

Dk Ndugulile  amesema katika kipindi cha 2018/19 mashauri 11,897 yaliripotiwa wakati mwaka 2017/18 kulikiwa na mashauri 11,815.

Katika swali la nyongeza mbunge wa Ulanga (CCM), Godluck Mlinga amehoji ni kwa nini Serikali isiweke sheria ya watoto wanapokwenda kliniki kwa mara ya kwanza kupimwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili  kujua baba zao. Amesema chanzo cha kutelekezwa kwa watoto ni wanaume kubambikiwa.

Katika majibu yake Dk Ndugulile amesema adhabu iliyowekwa kwa wanaotelekeza watoto inatosha na Serikali haioni sababu ya kubadili sheria hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz