Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wahimizwa kujikinga na magonjwa

4a4bdbf921b86ee80cbcfc55629006e5 Wananchi wahimizwa kujikinga na magonjwa

Sat, 20 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imewaomba wananchi kuchukua hatua mbalimbali, kujikinga na magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza na kufahamu kuwa kinga ni bora kuliko tiba kwani tiba ina gharama kubwa.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika mjini hapa.

Alisema kusema kuwa serikali kupitia waziri mwenye dhamana na afya imetoa agizo kuwa mwaka huu ni wa kuimarisha mifumo ya udhibiti na kinga kwa magonjwa hayo. Dk Rutatinisibwa alisema kuwa magonjwa mengi yakiwemo ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, yanazuilika kama kila mmoja atapata elimu juu ya magonjwa hayo na jinsi ya kuyazuia.

Alisema magonjwa ya kuambukiza yanasababishwa na vimelea vya bakteria, virusi, fangasi na wadudu mbalimbali na huambukizwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa njia mbalimbali.

Alifafanua kuwa mwenendo wa takwimu wa magonjwa ya kuhara, kipindupindu, homa kali ya mapafu, kifua kikuu, mafua, malaria, dengue, homa ya bonde la ufa, homa ya matumbo, unaonesha kuwa magonjwa hayo huongezeka kipindi cha kuanzia Novemba hadi Aprili kila mwaka.

Dk Rutatinisibwa alisema kuwa hali hiyo husababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa hasa mvua zinazoponyesha kwa wingi kipindi hicho, hivyo alishauri wananchi kuchukua tahadhari zote muhimu za kujikinga na magonjwa kama hayo.

Alisema dalili za magonjwa hayo zinaweza kuwa mafua, kikohozi, homa kali, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, maumivu ya mwili, kukosa hamu ya chakula, kushindwa kutambua harufu, kizunguzungu, kuharisha au kutapika.

Alisema kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza hayatokani na kuambukiza, bali ni ya muda mrefu na mfano wa magonjwa hayo ni moyo, shinikisho la damu la juu, kisukari, saratani, figo na pumu na baadhi yake yanaweza kuwa na dalili kama za magonjwa ya mfumo wa hewa. Alitaka maeneo ya kazi, shule, vyuo na nyumba za ibada, kuweka vitakasa mikono na watu wanawe mikono kwa maji yanayotiririka.

Pia alitaka wananchi kunasa mikono kabla ya kula chakula, baada ya chakula na wanapotoka chooni. Vifaa vya kunawia mikono viwepo maeneo yote ili kujikinga na magonjwa. Aliwataka waondokane na hofu, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kuvaa barakoa, kukaa umbali wa mita moja hadi mbili kwenye mikusanyiko.

Chanzo: habarileo.co.tz