Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi kulipa bima ya afya kwa awamu- Ummy

Ummy NHIF Wananchi kulipa bima ya afya kwa awamu- Ummy

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema kuwa dhamira ya huduma ya Bima ya Afya kwa wote inalenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma iliyobora na wananchi watalipia kwa awamu ili kuwezesha huduma hiyo muhimu katika maisha yao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali itahakikisha wananchi wanapata fursa hii ambayo ni muhimu katika familia na taifa kwa ujumla kama ilivyodhamira ya Serikali kwa watu wake.

“Dhamira ya Serikali kuhusu Bima ya Afya kwa Wote ni kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu kama Serikali ya kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma bora za Afya bila kikwazo cha kifedha na tutashauri kuwa wananchi walipie kiasi cha Shilingi 50,400/= ambayo wataweza kulipa kwa awamu nne kwa mwaka ili waweze kumudu na kupata huduma hii muhimu”, alisema Mhe. Ummy.

Aidha, Waziri Ummy alitoa rai kwa Watanzania kuwa wajiunge na huduma hiyo ambayo itawahakikishia ubora wa matibabu wakipatwa na matatizo ya kiafya. Mhe. Ummy aliongezea na kusema kitita cha msingi kitawekwa ambacho mwananchi atajipimia katika kupata huduma za msingi za afya kama vile vipimo vya Maabara, Radioloji na huduma zingine za msingi endapo mtu anapata changamoto ya kiafya.

Waziri Ummy aliongeza kuwa Serikali itaweka nguvu kubwa katika kutoa eilimu ili wananchi wajiunge na huduma hiyo ambayo baada ya kutungwa kwa sheria yake wataanza utekelezaji wake hatua kwa hatua ikiwemo kuanza na makundi maalum kama vile wanafunzi wa shule za kulala, watu wa Sekta Binafsi na akasisitiza kuzingatiwa kwa wasio na uwezo kupitia TASAF nao pia wapewe nafasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live