Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi watatu Mihayo Sekondari walazwa ICU

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora.Wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Mihayo, wamelazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum, ICU baada ya kuunguzwa na moto wakati mabweni ya shule hiyo yaliposhika moto.

Akizungumzia tukio hilo leo Agosti 29, kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema wanafunzi wengine saba pia wamelazwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Kitete na Mtakatifu Anna ya Ipuli.

Amesema kuwa wanafunzi waliolazwa ni miongoni mwa wanafunzi 54 waliopelekwa hospitali usiku kwa ajili ya kupata matibabu.

"Hali za wanafunzi walioruhusiwa kutoka hospitalini, zinaendelea vizuri,” amesema Kamanda Nley

Kamanda Nley amesema bado uchunguzi wa chanzo cha moto huo unaendelea.

Pia alishukuru ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa na wananchi pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

“Ni kweli kuwa wanafunzi wamepoteza mali zao katika tukio hilo ambalo ni la kwanza kutokea katika shule hiyo,” amesema.

Alibainisha kwamba hadi sasa bado thamani ya mali iliyoungua pamoja na majengo haijajulikana na tathmini inaendelea kufanyika.

Mkuu wa shule hiyo, Padri Salvatory Maganga amesema kuwa magodoro 131 yametekea pamoja na mali nyingine za wanafunzi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz