Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wa bweni hatarini kuambukizwa kifua kikuu

Kifuaakikuupic Data Ummy ametoa rai kwa wakuu wa wilaya ili kudhibiti kasi ya maambukizi

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imewataka wakuu wa wilaya nchini kushirikiana na waganga wakuu wa wilaya kuweka utaratibu wa kuzitembelea shule za bweni ili kubaini mlundikano wa wanafunzi katika mabweni hayo na kuchukua hatua ili kudhibiti maambukizi ya kifua kikuu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu (TB) duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Tanga.

Amesema kumekuwa na mlundikano mkubwa wa wanafunzi katika shule za bweni ambao unaweza kusababisha athari za kiafya kwa wanafunzi.

"Wekeni utaratibu wa kutembelea Kwenye shule za bweni na kuchukua hatua kwani maambukizi mengine yanapatikana huko mashuleni," amesema.

Pamoja na mambo mengine ametoa katazo kwa hospitali zote nchini kuacha tabia ya kutoza fedha kwa wanafunzi wanaokwenda kupima afya kwa ajili ya kujiunga na shule au vyuo kwani kwa kufanya hivyo wanakiuka utaratibu.

"Ni kosa kuchukua fedha kwa ajili ya ujazaji fomu ya uchunguzi wa afya kwa wanafunzi huduma hii ni bure hivyo wapimwe bure, siyo mnasaini bila kuwafanyia uchunguzi wa afya kama fomu inavyoelekeza kwa kufanya hivyo mnasababisha watoto kuambukizana maradhi," amesema Waziri Ummy.

Advertisement Aidha, amesema serikali imeandaa mpango wa kuwawezesha kiuchumi kaya masikini zinazohudumia wagonjwa wa kifua kukuu kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030 .

Amesema lengo la serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta binafsi kuutokemeza ugonjwa huo ambao mpaka sasa wagonjwa 47,000 bado hawajafikiwa.

Aidha Waziri Ummy ametoa agizo pia kwa waganga wakuu wote nchini kuwabaini wenye maduka makubwa ya dawa ambao wanauzia wananchi dawa kali bila cheti kutoka kwa mtabibu.

"Salamu ziwafikie wenye maduka makubwa ya dawa ninayo majina ya maduka makubwa mawili nimepata taarifa wanauza dawa kiholela kwa kutoa dawa kali ambazo hazitakiwi kutolewa bila cheti cha daktari nasema nitawachukulia hatua kali hili halikubaliki," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live