Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi Sumve kupewa semina ya VVU

2fc4d4fc51a29fea39c151984ec37b0a Wanafunzi Sumve kupewa semina ya VVU

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MRATIBU wa mradi wa Elimu ya Ukimwi kwa vijana,Sebastian Gregory amesema wapo katika mpango wa kuhakikisha wanatoa mafunzo ya Virusi vya Ukimwi kwa shule 20 za Sekondari kijiji ya Sumve wilayani Kwimba.

Rai hiyo alitoa wakati wa mafunzo malumu ya Vvu kwa walimu wa shule za Sekondari katika kata hiyo. Gregory alisema kupitia mradi huo watatembelea shule baadhi ya shule za Mushialage,Sumve,Nyamikoma,Mantare, Ishingisha na Bumengeja ambapo wanafunzi wa shule hiyo watafanyiwa vipimo vya vvu.

Amewataka watoa huduma wa vituo vya Afya kuepuka kutumia lugha zisizokuwa nzuri kwa wanafunzi walioathirika.

Mradi huo wa elimu ya Ukimwi kwa vijana unadhaminiwa na Ambassador’s Fund for HIV/AIDS relief.

Daktari kutoka Sumve hospitali Teule,Dk Abdallah Bihoga alisema kwa Takwimu za mwaka 2019 katika kata ya Sumve kuna watoto 114 wanaendelea na dawa kati ya miaka 0-14 na watoto 46 kati ya miaka 15-19 wanatumia dawa za kupunguza makali ya ARV.

Alisema muitikio wa vijana kwenye kliniki ya VVU ni mkubwa sana kutokana na vijana wamewekewa siku za wikiendi ambapo wanaudhuria kliniki.

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Bungulwa,Godfrey Mahimbo alisema uelewa wa walimu wengi jinsi ya kuishi vijana waliothirika na VVU bado ni mdogo sana.

Alisema kuna wakati walimu hutoa adhabu kwa wanafunzi wote shuleni bila kujali kuwa wanafunzi wengine ni waathirika.

Chanzo: habarileo.co.tz