Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 800 Mloganzila wanufaika na uchunguzi wa masikio

Wanafunzi 800 Mloganzila Wanufaika Na Uchunguzi Wa Masikio Wanafunzi 800 Mloganzila wanufaika na uchunguzi wa masikio

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga na Mloganzila imefanya uchunguzi wa magonjwa ya masikio kwa wanafunzi takribani 800 wa Shule ya Msingi Mloganzila ambapo kati ya hao asilimia 50 wamekutwa na changamoto ya nta iliyogananda kwenye masikio na asilimia 10 chanamoto za usikivu kutokana na nta au tatizo la mishipa.

Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Dkt. Jonas Ndasika na kuongeza kuwa kwa wale waliiokuwa na nta walitolewa na wale waliokutwa na changamoto za usikivu wamepewa rufaa ya kwenda Muhimbili-Mloganzila kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

"Leo pamoja na kufanya uchunguzi huu tumetoa elimu pia, tunawashauri wazazi wawe na utaratibu wa kuwapeleka watoto wao hospitalini kwa ajili ya uchunguzi hususani kipindi cha likizo ili kuepuka madhara zaidi yanayoweza kujitokeza ambayo yanaweza kuathiri mwenendo wa kitaaluma wa mwanafunzi husika,” ameongeza Dkt. Ndasika.

Kwa upande wake Mwalimu Kiongozi wa Shule ya Msingi Mloganzila, Mwalimu Jackson Massasi ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uamuzi wake wa kutoa elimu na uchunguzi kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Mwl. Massasi amebainisha kuwa MNH-Mloganzila imekuwa ikiisaidia shule hiyo katika mambo malimbali katika kuendeleza taaluma, ametaja misaada hiyo ni pamoja na ujenzi wa matundu 10 ya vyoo kwa wasichana na kusaidia sare kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.

Siku ya Usikivu Duniani huadhimishwa Machi,3 kila mwaka ambapo wataalam hutumia siku hiyo kutoa elimu na jamii uchunguzi wa magonjwa ya usikivu kwa lengo la kuondoa changamoto ya usikivu kwa jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live