Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamiminika kupima afya bure Mlonganzila

Tue, 13 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamia ya wananchi wameendelea kujitokeza kuchunguza afya bure katika Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani itakayofanyika jesho.

Magonjwa yanayochunguzwa ni kisukari, macho, lishe na meno lakini pia madaktari wanaohusika na kazi hiyo wanatoa ushauri endapo mtu anabainika na tatizo lolote.

Msimamizi wa kazi hiyo, Mkuu wa Kitendo cha Kisukari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Mohammed Juma amesema kazi hiyo itaendelea vizuri na utamalizika Ijumaa.

"Tulianza jana (Jumatatu) na mwisho ni Ijumaa. Tulijipanga kuhudumia watu zaidi ya 3,000 lakini huenda wakazidi kwani jana siku ya kwanza tu walikuja watu zaidi ya 290 leo mpaka sasa (saa 7:00 mchana) wameshakuja zaidi ya 200,” amesema Dk Mohammed.

Amesema lengo la kufanyia uchunguzi huo Mloganzila ni kulitangaza tawi hilo la MNH kwa watu kwani kumekuwapo na uvumi kwamba hakuna madaktari wa kutosha.

"Watu wamekuwa wakisema ukitolewa Muhimbili kuja huku unakuwa umepotea lakini sio kweli huku nako kuna huduma nzuri, madaktari wa kutosha na vifaa vya kisasa vipo.”

“Watu wanaletwa huku ili kupunguza msongamano kule hususani katika wodi ya wagonjwa wa uchunguzi," amesema Dk Juma.

Kwa upande wa wananchi waliohudhuria uchunguzi huo, wamesema huduma ni nzuri na wanahudumiwa kwa haraka.

"Huduma ni nzuri japo watu ni wengi lakini tunahudumiwa haraka na nina uwezo wa kumaliza hapa kwenye kisukari nikaenda kwenye meno bila mashaka," amesema Joseph Shoi (55) mkazi wa Mbezi.



Chanzo: mwananchi.co.tz