Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamiliki 719 wa maabara binafsi kikaangoni

34176 Pic+maabara Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imetangaza kuzifungia maabara 719 zilizopo katika vituo vya afya binafsi ifikapo Januari 15, 2019 na wamiliki wake watashtakiwa.

Uamuzi huo umetolewa kutokana na maabara hizo kutojiandikisha katika bodi ya usimamizi wa maabara binafsi za afya (PHLB) pamoja na kuwa na malimbikizo ya ada na tozo.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatatu Desemba 31, 2018 mkurugenzi wa tiba ya Wizara ya Afya, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi Septemba 2018, PHLB ilikuwa inazitambua maabara 641 zinazojitegemea na 719 zilizopo kwenye vituo vya tiba vya watu binafsi.

Dk Gwajima amesema bodi imebaini baadhi ya wamiliki wa maabara binafsi hususan zilizopo katika vituo vya tiba kutofuata maadili ya uwajibikaji kisheria.

Amesema hadi Septemba 2018, kati ya vituo vya tiba 1,713 vya watu binafsi vyenye maabara ndani,  ni maabara 1,012 sawa na asilimia 58 ndizo zilizotimiza wajibu wa kujiandikisha kwenye bodi hiyo.

“Tunaagiza watimize wajibu wao bila shuruti tena pasipo kuendelea kuisababishia Serikali gharama za ziada za kuwafuatilia. Ifikapo Januari 5, 2019 ambaye hajatimiza wajibu wake atafungiwa bila taarifa ya ziada na kushtakiwa,” amesema Dk Gwajima.

“Kila mmiliki ahakikishe amelipa ada na tozo stahiki ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya nyuma na faini zote stahiki na amepata risiti halali za malipo hayo.”



Chanzo: mwananchi.co.tz