Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliowekewa nyonga bandia wafunguka

Nyonga Gsrs Waliowekewa nyonga bandia wafunguka

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wagonjwa walionufaika na matibabu ya upasuaji wa nyonga yaliyotolewa na jopo la madaktari wa mifupa na nyongo kutoka Los Angeles, Marekani Agosti mwaka huu kupitia mpango wa 'Samia Love', wameelezea hali zao baada ya upasuaji huo.

Wakizungumza katika mahojiano maalum leo Jumatatu Septemba 11, 2023, wamesema hali zao zimebadilika kwa kiasi kikubwa mara baada ya upasuaji huo baada ya kuishi katika baiskeli za kutembelea na maumivu makali kwa muda mrefu.

Madaktari hao 60 waliobobea katika tiba ya mifupa, nyonga na mishipa ya fahamu waliwaona na kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa takribani 200 ikiwa ni pamoja na kuwafanyia upasuaji wa nyonga na goti wagonjwa 51 katika Hospitali ya Selian inayomilikiwa na Kanisa la Kiiinjili la Kilutheri Tanzania iliyopo jijini Arusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live